Kansela Scholz akiri ushindi wa AfD watia wasiwasi
2 Septemba 2024Chama cha Mbadala wa Ujerumani ama AfD kimekuwa cha kwanza cha mrengo mkali wa kulia kushinda uchaguzi wa jimbo nchini Ujerumani tangu Vita vya Pili vya Dunia, kufuatia ushindi kwenye jimbo la Thuringia jana Jumapili. Kwenye jimbo la Saxony chama hicho kimeshika nafasi ya pili.
Scholz aliyezungumza kama mbunge wa chama chake cha Social Democrats, SPD, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba matokeo ya AfD huko Saxony na Thuringia yanatia wasiwasi na kulionya taifa kuwa hilo haliwezi kukubalika, akisema chama AfD inaivuruga nchi, kudidimiza uchumi, kuigawa jamii na kuharibu sifa ya Ujerumani.
Soma pia:Wajerumani weusi wahofia ushindi wa AFD majimbo ya mashariki
Hata hivyo, AfD kinachotajwa na idara ya usalama wa taifa nchini Ujerumani kama cha mrengo mkali wa kulia, bado hakiwezi kuunda serikali kwa kuwa vyama vingine hadi sasa vimekataa kushirikiana nacho.