1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSaudi Arabia

Saudi Arabia kusaini makubaliano ya dola mil. 500 na Afrika

10 Novemba 2023

Wakfu wa Maendeleo wa Saudi Arabia unatarajiwa kusaini makubaliano ya thamani ya dola milioni 533 na mataifa ya Afrika.

https://p.dw.com/p/4Ye0T
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman. Taifa hilo la kifalme limeahidi kufadhili miradi mbalimbali barani Afrika
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman. Taifa hilo la kifalme limeahidi kufadhili miradi mbalimbali barani Afrika Picha: Leon Neal/empics/picture alliance

Waziri wa fedha wa Saudi Arabia Mohammed al-Jadaan amesema hayo jana kwenye Kongamano la Kiuchumi kati yao na Afrika.

Jadaan aidha amesema pamoja na washirika wao wanaangazia namna ya kuisaidia Ghana na mataifa mengine yaliyoelemewa na madeni.

Waziri wa uwekezaji wa Saudi Arabia Khalid Al-Falih alisema zaidi ya dola bilioni 700 za Mfuko wa Uwekezaji wa Umma, zitasaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya uwekezaji barani Afrika.

Naye waziri wa nishati Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman kwenye mkutano huo alisaini makubaliano ya awali na Nigeria, Senegal, Chad na Ethiopia ya kushirikiana katika masuala ya nishati.

Msumbiji nayo ilisaini makubaliano ya ufadhili wa dola milioni 158 na Wakfu wa Maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ambayo ni pamoja na hospitali na bwawa.