1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ronaldo "hauzwi"

11 Julai 2022

Kocha mpya wa Machester United Erik ten Hag amesema Jumatatu hii kwamba Cristiano Ronaldo hauzwi licha ya kushindwa kujiunga na wenzake kwenye ziara ya kabla ya kuanza kwa msimu, nchini Thailand na Australia.

https://p.dw.com/p/4DxKm
Champions League - Young Boys Berne v Manchester United - Christiano Ronaldo
Picha: Lairys Laurent/ABACA/picture alliance

Erik ten Hag akizungumza kabla ya mechi ya kirafiki ya kabla ya kuanza msimu dhidi ya Liverpool huko Bangkok, amesema "Tuna mipango na Christiano Ronaldo kwa msimu ujao na huo ndio msimamo na ninatarajia kufanya kazi naye". "Nimesoma. Lakini kile ninachoweza kusema ni kwamba Cristiano hauzwi. Yuko kwenye mipango yetu na tunataka kufanikiwa tukiwa pamoja", aliongeza Ten Hag.

Kulingana na meneja huyo raia wa Uholanzi, tayari alishazungumza na mshambuliaji huyo kabla ya kusambaa kwa ripoti wiki iliyopita kwamba anataka kuondoka na kusema kwamba walikuwa na mazungumzo mazuri tu.

Ronaldo pia hakuhudhuria mazoezi ya awali na klabu hiyo ya Premier wiki iliyopita kwa madai ya matatizo ya kifamilia, huku ripoti zikisema Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 anataka kuondoka United baada ya kikosi hicho kushindwa kufuzu kwenye michuano ya Mabingwa Ulaya, lakini pia matokeo mabovu tangu aliporejea mwaka jana.

United ilimaliza ikiwa nafasi ya sita kwenye msimu uliopita. Ronaldo alifunga magoli 24.

Mashirika: AFPE