1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa aisifia miaka 30 ya utawala wa ANC

9 Februari 2024

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametumia hotuba yake kwa taifa kuelezea mafanikio ya chama chake katika kipindi cha miaka 30 ingawa hakuelezea kwa kina mipango ya kushughulikia changamoto zinazolikabili taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4cDB5
Rais Matamela Cyril Ramaphosa
Rais Matamela Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.Picha: Karim Sahib/AFP/Getty Images

Ramaphosa alizungumzia mafanikio ya chama chake cha African National Congress (ANC) katika hotuba muhimu mbele ya bunge siku ya Alkhamis (Februari 8).

Aliitaja ANC kama chama kilichoiongoza Afrika Kusini kuzivuuka salama changamoto kama vile janga la UVIKO-19 na ufisadi uliokithiri na kuongeza kuwa miaka mitano iliyopita ilikuwa ni ya "kujijenga na kuanza upya."

Soma zaidi: Kurudi kwa Zuma urais ANC

Chama cha ANC kilichotawala tangu uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1994 chini ya Nelson Mandela, kitakabiliwa na upinzani mkali katika kampeni za uchaguzi utakaofanyika kati ya Mei na Agosti, huku kukiwa na dalili za kupoteza uwingi wa viti bungeni.