1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Rais wa Ukraine amtunuku Baerbock Nishani ya Juu

6 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemtunukia Nishani ya Juu ya "Order of Merit" Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock kutokana na mchango wake nchini humo.

https://p.dw.com/p/4av2K
Ukraine Kyiv | Mawaziri wa Mambo ya Nje Baerbock na Kuleba
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena baerbock alipokutana mjini Kiev na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Kiev, 10 09 2022 Kiev Ukraine.Picha: Thomas Trutschel/photothek/IMAGO

Wabunge wa Bunge la Ujerumani Marie-Agnes Strack-Zimmermann na Anton Hofreiter pia walitunukiwa nishani kutokana na uungaji mkono wa kuisaidia Ukraine.

Kwenye amri iliyotolewa muda mfupi kabla ya mwaka mpya, Rais Zelensky aliwatunuku watu wengine 32 kutokana na mchango wao binafsi na mkubwa wa kuimarisha uhusiano na taifa hilo na kuunga mkono mamlaka na uadilifu wa Ukraine.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez na Waziri Mkuu wa Albania, Edi Rama, walitunukiwa nishani ya Juu kabisa ya Yaroslav.