Rais William Ruto atimiza mwaka mmoja madarakani
13 Septemba 2023Matangazo
Hadi sasa, wakenya wanalalamikia ughali wa maisha kutokana na ongezeko la bei za bidhaa na mafuta ya petroli.
Serikali hiyo ya Kenya inashikilia kwamba imefanikiwa kuurekebisha uchumi kwa misingi ya kulipunguza deni baada ya kuongeza mapato ya kodi kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2023.
Rais Ruto awaomba wapinzani Kenya kutoa nafasi kwa mazungumzo
Mapema mwezi wa Agosti mwaka huu, Rais William Ruto alishikilia kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki haiwezi kuongozwa kwa kutegemea mikopo na kwahivyo hatua za kuongeza kodi ili kuimarisha pato la taifa ni ya lazima.Upinzani unaoongozwa na Raila Odinga bado hauna imani na serikali hiyo ya Kenya.