1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSri Lanka

Rais Wickremesinghe aidhinishwa kugombea urais Sri Lanka

15 Agosti 2024

Tume ya uchaguzi ya Sri Lanka imemuidhinisha Rais Ranil Wickremesinghe kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 21.

https://p.dw.com/p/4jUSm
Rais Ranil Wickremesinghe kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 21
Rais Ranil Wickremesinghe kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 21Picha: Eranga Jayawardena/AP/picture alliance

Wickremesinghe alikuwa miongoni mwa wagombea 39 waliowasilisha maombi yao ya kugombea katika uchaguzi huo muhimu utakaoamua jinsi Sri Lanka itakavyojiondoa kutoka kwenye mzozo huo, uliotokana na nchi hiyo kumaliza akiba zake za nchi za nje na kusababisha uchumi kuporomoka na hatimaye kufika hatua ya kushindwa kulipa deni lake mwaka 2022.

Wickremesinghe, kiongozi wa upinzani Sajith Premadasa na mbunge anayefuata nadharia za kisiasa za Karl Marx, Anura Kumara Dissanayake, wanaonekana kama wagombea walio katika mstari wa mbele.