1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSri Lanka

Polisi waapa kupambana na madawa ya kulevya Sri Lanka

14 Januari 2024

Polisi nchini Sri Lanka wamesema katika msako unaoendelea wa kupambana na dawa za kulevya nchini humo wataendelea kuwakamata watu wanaoshukiwa kuhusika na biashara hiyo ya mihadarati nchini humo.

https://p.dw.com/p/4bDdw
Kupamabana na madawa ya kulevya changamoto kubwa Sri Lanka
Kupamabana na madawa ya kulevya changamoto kubwa Sri LankaPicha: Akila Jayawardana/picture alliance/NurPhoto

Msako huo umelaaniwa na Umoja wa Mataifa, wakati ambapo maelfu ya watu tayari wanashikiliwa na polisi.

Polisi nchini Srilanka imetoa kauli hiyo siku mbili baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu kuikosoa operesheni hiyo ya polisi na kusema kuwa ni ya ukandamizaji kwa kuendesha upekuzi ambao haujaidhinishwa, ukamataji ovyo wa watu na kuwaweka kizuizini, pamoja na mateso mengine.

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia haki za binadamu Volker Turk, ameitaka serikali ya Sri Lanka kuiangalia upya operesheni hiyo na kurekebisha mbinu zinazozingatia haki za binadamu katika msako wa kupambana na dawa za kulevya.

Takriban watu 30,000 wamekamatwa tangu kuanza operesheni hiyo ya polisi mnamo mwezi Desemba,mwaka uliopita.