1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili mjini Athens

7 Desemba 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili Athens kwa ajili ya mazungumzo na wenzake wa Ugiriki huku mataifa hayo mawili yakiwa na matumaini ya kuanza ukurasa mpya wa mahusiano baada ya mivutano ya miaka kadhaa.

https://p.dw.com/p/4ZrkT
Erdogan Besuch Deutschland
Picha: DHA

Ugiriki na Uturuki ambayo yote ni wanachama wa jumuiya ya kijeshi ya NATO yamekuwa yakivutana kutokana na masuala kadhaa ambayo ni pamoja na rasilimali za nishati.Kwenye mikutano ya maafisa hao kunatarajiwa kufikiwa azimio na makubaliano katika sekta mbalimbali kuanzia za uchumi, afya, elimu, kilimo, uhamiaji na utalii, wamesema maafisa wa serikali.Erdogananatarajiwa kukutana na Rais wa Ugiriki Katerina Sakel faro poulou na Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis na utakuwa ni mkutano wa tatu tangu mwezi Julai, wakati walipokubaliana kurejesha mazungumzo ya ngazi zote.