1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani Steinmeier akutana na Erdogan mjini Ankara

24 Aprili 2024

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amekutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwa katika ziara yake ya siku tatu mjini Ankara.

https://p.dw.com/p/4f90m
Ankara | Steinmeier na Erdogan
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akiwa na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Erdogan alimkaribisha mgeni wake kutoka Ujerumani kwa heshima za kijeshi, kabla ya kukaa kwa mazungumzo ya kina yanayotarajiwa kujikita zaidi katika mzozo wa Gaza ambao umeziweka Ujerumani na Uturuki katika misimamo tofauti. Ujerumani imekasirishwa na msimamo wa Erdogan wa kuliunga mkono kundi la wanamgambo la Hamas.

Wakimbizi wateswa Uturuki

Rais Steinmeier pia anatarajiwa kuzungumzia suala la hali ya haki za binadamu nchini Uturuki.Shirika la waandishi habari wasiokuwa na mipaka lilimuomba   rais huyo wa Ujerumani kabla ya ziara yake kuishinikiza serikali ya Uturuki iwaachilie huru waandishi habari wanaozuiliwa  jela nchini humo.