1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tunisia amwajibisha waziri kuhusu vifo vya mahujaji

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Rais wa Tunisia Kais Saied amemfuta kazi waziri wa masuala ya kidini Ibrahim Chaibi kufuatia vifo vya mahujaji 49 wa nchi hiyo katika Hijja ya mwaka huu nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4hOGD
Saudi Arabia| Mahujaji
Mahujaji kutoka nchi tofauti wakiwa mjini MeccaPicha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Rais wa Tunisia Kais Saied amemfuta kazi waziri wa masuala ya kidini Ibrahim Chaibi kufuatia vifo vya mahujaji 49 wa nchi hiyo katika Hijja ya mwaka huu nchini Saudi Arabia.Nani wakulaumiwa au nini kilichosababisha vifo vya Mahujaji huko Makka?

Uamuzi huo umechukuliwa muda mchache baada ya waziri Chaibi kuthibitisha vifo vya Watunisia 49 hasa kutokana na joto kali wakati wa Hijja. Waziri huyo alisema vifo vya watu 44 vilikuwa vya mahujaji ambao hawakusajiliwa, waliokuwa wamesafiri kwa kutumia vibali vya utalii. Mahujaji zaidi ya 600 wafa kwenye ibada ya Hija

Waziri huyo alikiri uwezekano wa kutokea uzembe katika kuwashughulikia mahujaji, hayo ikiwa ni kulingana na ripoti ya shirika la habari la TAP. Hali ya joto kali katika mji wa Saudia wa Makka na maeneo mengine matakatifu ilifikia nyuzi joto 50 katika kipimo cha Celsius siku ya Jumanne wiki hii ambayo ndio ilikuwa mwisho wa Hijja.