1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahujaji zaidi ya 600 wafa kwenye ibada ya Hija

19 Juni 2024

Mwanadiplomasia mmoja nchini Saudi Arabia leo amesema kwamba raia 68 wa India wamefariki dunia wakati wa kuhiji mwaka huu kutokana na joto kali na kupelekea idadi jumla ya watu waliofariki kufikia zaidi ya 600.

https://p.dw.com/p/4hGLm
Saudi Arabia Mina
Mmoja wa mahujaji wa mwaka 2024 akiwa kwenye eneo la Mina.Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Mwanadiplomasia huyo, ambaye hakutaka kutambulishwa, amesema mbali na joto kali, baadhi ya mahujaji wamefariki kutokana na sababu za kawaida na wengine wengi walikuwa na wazee.

Idadi hii mpya inakuja baada ya wanadiplomasia wawili wa Kiarabu kuliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne (Juni 18) kwamba vifo 550 vimerekodiwa wakati wa Hija, hiyo ikiwa na mojawapo ya nguzo tano za dini ya Kiislamu ambayo Waislamu wote walio na uwezo wanastahili kuitekeleza angalau mara moja maishani mwao.

Mataifa mengine yaliyothibitisha viofo vya raia wake ni pamoja na Misri, Jordan, Iran, Senegal, Tunisia na eneo lenye mamlaka ya ndani kaskazini mwa Iraq, Kurdistan.

AFP inasema idadi jumla ya waliofariki kwa sasa ni watu 645.