Al-sisi afanya ziara ya kwanza Uturuki tangu achaguliwe
4 Septemba 2024Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi atafanya mazungumzo na rais Tayyip Erdogan nchini Uturuki leo ambako anafanya ziara yake ya kwanza, tangu miaka 12 kama kiongozi wa Misri, baada ya kurejea mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.
Ziara ya Al Sisi, Uturuki inafanyika kufuatia ziara iliyofanywa na Erdogan mjini Cairo mwezi Februari, ambayo ilikuwa ya kwanza tangu mwaka 2012 na ambayo ilifunguwa hatua kubwa ya kujengwa upya mahusiano yaliyokuwa yameharibika kwa muongo mzima.
Soma pia: Rais El Sissi azuru Uturuki baada ya kumaliza ya muongo mmoja madarakani
Viongozi hao wawili watajadili kuhusu mahusiano ya nchi hizo lakini pia watashauriana juu ya masuala kadhaa yanayoendelea kwa sasa kikanda na kimataifa na hasa kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya ardhi ya Wapalestina.