Rais wa Iran aanza ziara China,makubaliano kadhaa kuafikiwa
14 Februari 2023Matangazo
Raisi atafanya mazungumzo na mwenzake wa China, Xi Jinpingkatika mji mkuu Beijing, ambapo wawili hao wanatarajiwa kusaini nyaraka kadhaa za ushirikiano.
Iran na China zina uhusiano imara wa kiuchumi, hasa katika nyanja za nishati, usafiri, kilimo, biashara na uwekezaji, na mwaka 2021 zilisaini mkataba wa miaka 25 wa ushirikiano wa kimkakati.
Soma pia:Rais wa Iran kufanya ziara nchini China
Mataifa hayo yote mawili yanakabiliwa na shinikizo kutoka Marekani kuhusiana na misimamo yao kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku Iran ikiwa imewekewa vikwazo na Marekani kutokana na mpango wake wa nyuklia.