1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China: Marekani yakiuka kanuni za uchumi wa soko na sheria

10 Februari 2023

China imesema Marekani inakiuka kanuni za soko kwa kuwazuia Wachina kununua mali zisizohamishika.

https://p.dw.com/p/4NK1R
China Peking 2022 | Mao Ning, Sprecherin des Außenministeriums
Picha: Kyodo/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema Marekani inakwenda kinyume na kanuni za uchumi wa soko na sheria za kibiashara za kimataifa kwa zingatio la kuwapiga marufuku raia wa China kununua mali zisizohamishika nchini Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika utaratibu wake wa kawaida, msemaji wa wizara hiyo Mao Ning amesema kimsingi dhana ya kile kinachoelezwa kuwa ni usalama wa taifa na kuingiza siasa katika masuala ya kiuchumi na uwekezaji kunaleta matokeo hayo ya ukiukwaji.

Msemaji Mao alikuwa akijibu swali kuhusu mipango ya majimbo ya Texas na Florida yenye kuzingatia kupiga marufuku raia wa China kununua mali.