Rais Tebboune ashida muhula wa pili Algeria
14 Septemba 2024Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameshinda muhula wa pili kwa asilimia 84.3 ya kura katika uchaguzi wa wiki iliyopita, kwa mujibu matokeo ya mwisho yaliyotangazwa. hata hivyo, matokeo hayo ni chini ya hesabu za makadirio ya awali yaliyopingwa na wapinzani.
Matokeo ya awali yaliyotolewa na mamlaka ya uchaguzi ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, ANIE, wiki iliyopita yalimpa Tebboune karibu asilimia 95 ya uungwaji mkono, na hivyo kusababisha wagombea wengine kupinga matokeo hayo katika rufaa zao kwenye Mahakama ya Kikatiba.
Soma zaidi.Wagombea wawili wa uchaguzi Algeria wapinga matokeo mahakamani
Rais wa mahakama hiyo ya kikatiba, Omar Belhadj, ametangaza hii leo katika televisheni na redio ya taifa matokeo rasmi yaliyompa ushindi Tebboune na kuwabwaga wapinzani wake wawili.
Hata hivyo, Ilitarajiwa kuwa Abdelmadjid Tebboune angelichaguliwa tena kwa muhula mwingine.