1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Abdelmadjid Tebboune ashinda muhula wa pili Algeria

9 Septemba 2024

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amechaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kwa kupata asilimia 95 ya kura baada ya uchaguzi uliofanyika siku Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4kPhV
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune.Picha: Presidenza Del Consiglio/Planet Pix/Zuma/picture alliance

Matokeo hayo yametangazwa jana jioni na mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo Mohamed Charfi.

Tebboune mwenye umri wa miaka 78 alitarajiwa kuibuka mshindi wa uchaguzi huo aliokuwa akichuana dhidi ya mgombea anayeegemea sera za dini ya kiislamu Abdelaali Hassani na msoshalisti Youcef Aouchiche.

Tebboune alitumia kampeni yake kuwahimiza wapigakura kujitokeza kwa mwingi kwenye uchaguzi wa mwaka huu akilenga kuifuta rikodi ndogo ya wapigakura katika uchaguzi uliomwingiza madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2019. Hata hivyo hadi sasa takwimu kamili za wapigakura walioshiriki uchaguzi hazijatolewa.

Wapinzani wa Tebboune pia wamelalamikia uwepo wa hitilafu kwenye zoezi la kuhesabu na kujumlisha kura.