Rais Museveni wa Uganda aongoza mkutano kuhusu Somalia
27 Aprili 2023Mkutano huu wa viongozi ni kilele cha vikao vya siku tatu ambavyo vimefanyika Kampala tangu siku ya Jumanne ambapo mawaziri wa ulinzi na masuala ya kigeni pamoja na wajumbe wa ngazi za juu Umoja wa Afrika na jumuiya ya wafadhili wamehudhuria. Washiriki ni kutoka kutoka mataifa ya Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Uganda na Somalia.
Soma Pia: Guterres asema Somalia ´inalipa gharama´ ya Mabadiliko ya Tabianchi
Katika vikao vyao, washiriki wamekubaliana kuendelea na utaratibu wa kuyaondoa majeshi yao wakisema kuwa ni hatua muhimu ili kuepusha kuzorotesha mafanikio waliopata kuhusiana na suala zima la amani usalama na uthabiti nchini Somalia. Katibu wa kudumu wa wizara ya masuala ya kigeni Uganda Vincent Bagiire ndiye alisoma taarifa ya pamoja ya wajumbe.
Awamu ya kwanza itakayomalizika tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu inalenga kuwaondoa wanajeshi walinda amani 2,000. Kulingana na wadau, wana imani kuwa jeshi la Somalia sasa lina uwezo wa kuhakikisha, amani na usalama katika nchi hiyo. Hata hivyo, naibu katibu mkuu wa umoja mataifa anayeshighulikia usalama Dkt. Aisa Kirabo Kacyira amehimiza mataifa ya kigeni kuendelea kutoa misaada muhimu kwa jeshi la Somalia wakati majeshi ya Umoja wa afrika chini ya mpango ujulikanao kama ATMIS wakiondoka. Mkuu wa ujumbe wa Ulaya nchini Uganda Jan Sadek amekubaliana na mwito huo akisema kuwa misaada itakuwa nyeti katika kuleta amani ya kudumu Somalia na kuepusha maovu kama vile ugaidi kanda hiyo ya Afrika. Katibu wa kudumu wa wizara ya masuala ya kigeni wa Uganda Vincent Bagire amesema.
Soma pia: UN: Zaidi ya Wasomali 140,000 wakimbia makwako kutokana na msimu wa mvua za mafuriko
Changamoto kubwa inayokumba mpango huo imeelezewa kuwa uhaba wa fedha kuutekeleza kwani Umoja wa Afrika unahitaji kiasi cha dola milioni kumi na moja hivi kuundesha.
Hadi wakati wa kuandaa taarifa hii, mkutano wa viongozi wa mataifa hayo ulikuwa unaendelea akihudhuria pia rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.