JamiiSomalia
UN: Zaidi ya Wasomali 140,000 wakimbia mafuriko
14 Aprili 2023Matangazo
Takwimu hiyo imetolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia migogoro, ikionesha kwamba jumla ya watu 170,000 wameathirika na mafuriko huku mikoa ya Kusini ya Gedo na Bay yakiwa yameathirika zaidi.
Mafuriko hayo yametokana na msimu wa mvua ambao kwa kawaida huanza mwezi Machi na kundelea hadi mwezi Juni katika eneo hilo la upembe wa Afrika.
Hali ya hewa huenda ikasababisha matatizo zaidi ya hali ya kibinadamu. Hivi sasa Somalia inakabiliwa na maambukizi ya kipindupindu na maradhi mengine yanayoambukiza kupitia maji machafu.