Rais Mattarella wa Italia alaani mauaji ya Balozi wake DRC
22 Februari 2021Balozi huyo Luca Attanasio ameuawa pamoja na watu wengine wawili katika shambulio baya lililofanywa dhidi yao na kundi la waasi wenye bunduuki lililoushambulia msafara wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP uliokuwa ukielekea wilayani Rutshuru.
Kwa mujibu wa vyanzo vyengine Balozi Attanasio alikufa kutoka na majeraha sambamba na dereva mmoja na mlinzi mmoja wa msafara huo.
Milio ya bunduki iliendelea kusikika katika maeneo ya kilimanyoka na Kanyamahoro katika mbuga ya wanyampori ya virunga, hali iliyo sababisha wasiwasi mkubwa kwa wakaazi waishio kandoni na mbuga hiyo. Carly Nzanzu Kasivita ni Gavana wa kivu ya kaskazini aliye thibitisha vifo vya watu hao.
Kulingana na wachambuzi wa maswala yakiusalama mashariki mwa Congo wanahofu kuwa mauwaji haya yanaweza kuwa na matokeo mabaya sana kwa wananchi katika tarafa za Rutshuru na Nyiragongo ambamo maelfu ya wakaazi huishi katika hali ya ukimbizi kufuatia ongezeko la makundi ya waasi nakutegemea kwa asilimia kubwa misaada kutoka nje.
Italia yasikitishwa na kifo cha balozi wake
Huku hayo yakiarifiwa, Waziri Mkuu wa Italia, Mario Draghi, ameelezea masikitiko yake makubwa kutokana na mauaji hayo, akisema kuwa jamhuri nzima inaomboleza vifo vya watumishi hao wa umma.
Jeshi nchini Kongo linasema linawasaka waliohusika na mauaji hayo.
Mara kadhaa vyombo vya usalama vimekuwa vikikosolewa vikali na wakaazi kwakushindwa kuimarisha ulinzi kwenye barabara hii kutoka Goma hadi rutshuru katika mbuga hii ambayo inayahifadhi makundi ya waasi ikiwemo hao kutoka nchi jirani ya Rwanda wa FDLR, hawa hapa ni wakaazi wa Goma wakionesha wasiwasi wao baada ya kifo cha Balozi Luca Attanasio.
Hadi tukienda hewani, jeshi la jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo,FARDC linaendesha msako mkali katika mbuga ya virunga kwenye eneo la tukio ili kuwatafuta walioyafanya mauji hayo.
Zaidi ya watu 20 waliripotiwa kuawa katika mbuga hii ya virunga mwaka uliopita baadhi yao wakiwa ni walinzi wa Mbuga.
Mwandishi: Benjamin Kasembe