Raia wa Venezuela kuanza maandamano mapya wikiendi hii
3 Agosti 2024
Venezuela inajiandaa kwa maandamano mapya kuendelea kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Nicolas Maduro wakati ambapo idadi ya mataifa yanayomtambua mpinzani wake Gonzalez Urrutia kuwa ndiye mshindi wa kweli wa uchaguzi wa Venezuela ikizidi kuongezaka.
Wote Maduro na upinzani wakiongozwa na mpinzani Maria Corina Machado wameitisha maandamano wikiendi hii kufuatia matokeo ya kura ya juma lililopita ambayo mpaka sasa yameleta utata nchini humo.
Mamlaka ya uchaguzi ya nchi hiyo ya Amerika Kusini (CNE) ambayo inatajwa kuwa ni tiifu kwa Maduro, siku ya Ijumaa ilimtangaza rasmi kuwa mshindi kwa asilimia 52 ya kura na kusema Gonzalez Urrutia amepata asilimia 43 ya kura.
Mataifa ya Marekani, Argentina, Costa Rica, Ecuador, Panama na Uruguay yamesema yanamtambua mpinzani Gonzalez Urrutia kama rais mteule wa kweli na siyo Nicolas Maduro.