1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Urusi, Iran na Uturuki zina mchango muhimu Syria

20 Julai 2022

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema nchi yake pamoja na Uturuki na Iran zina dhima kubwa katika kuunda mustakabali wa Syria na zinapaswa kupinga malengo ya mataifa ya magharibi kuigawa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4EOs4
Wladimir Putin trifft Ali Khamenei und Ebrahim Raisi in Teheran
Picha: tasnim

Putin na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan walikuwa mjini Tehran siku ya Jumanne kwa ajili ya mazungumzo na mwezao wa Iran Ebrahim Raisi, juu ya hali nchi Syria, lakini vita nchini Ukraine, mzozo juu ya usafirishaji wa nafaka za Ukraine na makubaliano ya nyuklia ya Iran ni mada zilizojadiliwa pia.

Rais Ebrahim Raisi alitowa wito wa kutafutwa suluhisho la kidiplomasia juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyvodumu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, ambalo linalinda mamlaka ya mipaka ya taifa hilo na kuwaruhusu Wasyria kuamua hatma yao ya kisiasa, huku Putin akitoa wito wa umoja zaidi katika sera ya Syria na kuyashutumu mataifa ya magharibi kwa uingiliaji.

Soma pia: Iran, Uturuki, Iran zatiliana saini mikataba ya kibiashara, kiuchumi

"Uingiliaji wa uharibifu wa mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani unachangia hilo kwa kiasi kikubwa hali ya wasiwasi katika maeneo yasiyo chini ya udhiti wa serikali.

Ni vyema kuchukua hatua za ziada katika muundo wetu wa pande tatu ili kuleta utulivu katika maeneo hayo na kuyarejesha chini ya udhibiti wa serikali ya Syria," alisema Putin mjini Tehran.

Iran Russland Türkei | Dreiergipfel | Wladimir Putin, Ebrahim Raisi und Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Urusi Vladmir Putin (kulia), Rais wa Iran Ebrahim Raisi, na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) wakati wa mkutano wa kilele wa pande tatu mjini Tehran, Julai 19, 2022.Picha: Iranian Presidency via ZUMA Press Wire/Zumapress/picture alliance

Urusi na Iran zote zinaunga mkono utawala wa rais wa Syria Bashar al-Assd, huku Uturuki ikiendeleza mafungamano na vikosi vya upinzani nchini humo.

Tangu mwaka 2017, Urusi, Iran na Uturuki zimedhamini mikutano chini ya kile kinachoitwa mfumo wa Astana, kwa lengo la kufikia muafaka wa kisiasa kumaliza vita hivyo.

Soma pia: Putin, Erdogan, Raisi wakutana Tehran

Uturuki ilisema hivi karibuni kwamba inatafakari kufanya mashambulizi mapya ya kijeshi kaskazini mwa Syria kuyalenga makundi ya silaha ya Kikurdi.

Tayari Ankara inadhibiti maeno makubwa ya Syria, lakini Urusi na Iran vimeitahadharisha Ankara dhidi ya kufanya mashambulizi mapya.

Kiongozi wa juu ya Iran Ayatollah Ali Khamenei alionya Jumanne kwamba mashambulizi yoyote ya Uturuki kaskazini mwa Syria yatawasaidia tu magaidi nchini humo.

Putin aishukuru Uturuki kwa upatanishi

Safari ya Tehran ndiyo ilikuwa ziara ya pili rasmi ya Putin tangu vikosi vya Urusi vilipoivamia Ukraine mwishoni mwa mwezi Februari.

Iran Russland Türkei | Dreiergipfel | Wladimir Putin, Ebrahim Raisi und Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Urusi Vladmir Putin (kulia) akiwa katika mazungumzo na mwenzake wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan mjini Tehran, Julai 19, 2022.Picha: Sergei Savostyanov/TASS/dpa/picture alliance

Wakati wa mkutano wake wa rais Erdogan, Putin alitoa shukuran zake kwa juhudi za upatanishi za Uturuki ili kuwezesha usafirishaji wa nafaka kutoka bandari za Ukraine kwenye bahari Nyeusi, ambako tani na tani zimekwama hivi sasa na kusababisha kupanda kwa bei za chakula kwenye masoko kote duniani.

Soma pia: Zelenskiy ataka Urusi itimuliwe FAO

Putin alisema ingawa masuala yote hayajaweza kutatuliwa, kumekuwa na maendeleo. Serikali mjini Kyiv na mataifa ya magharibi yanaituhumu Urusi kwa kuzuwia bandari nchini Ukraine, madai ambayo Moscow inayakanusha.

Iran imeendeleza msimamo rasmi wa kutoegemea upande kuhusu vita vya Ukraine, lakini huruma ya Tehran kwa Urusi inajulikana vyema, kutokana na ukweli kwmaba Moscow ndiyo muuzaji wake mkuu wa zana za kijeshi.

Chanzo: Mashirika