Putin kufanya ziara ya nadra ya siku mbili Korea Kaskazini
17 Juni 2024Putin anatarajiwa kukutana na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un kwa mazungumzo yatakayojikita katika kutanua ushirikiano wao wa kijeshi huku wakiungana zaidi hasa kufuatia mivutano ya mataifa hayo mawili na Marekani.
Shirika la habari la Korea limesema Putin atakuwepo nchini humo Jumanne na Jumatano baada ya kupata mualiko rasmi kutoka kwa Kim Joun Un.
Soma pia:Kim ausifu uhusiano unaotanuka wa Korea Kaskazini na Urusi
Ziara hiyo inakuja wakati kukiwa na wasiwasi wa kimataifa kuhusu silaha zinazotolewa na Pyongyang kwa Moscow, kuisaidia katika vita vyake na Ukraine ili kupata usaidizi wa kiuchumi na teknolojia itakayoimarisha kitisho cha kim cha silaha za nyuklia na mipango ya makombora.
Ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili umeongezeka hasa baada ya kim kufanya ziara Urusi na kukutana na Putin mwa mara ya kwanza tangu walipokutana mwaka 2019.