SiasaKorea Kusini
Korea Kusini kusitisha makubaliano ya kijeshi na Pyongyang
3 Juni 2024Matangazo
Baraza la Usalama la Korea Kusini, NSC limesema hii leo kwamba limeamua kuyasitisha makubaliano hayo hadi kutakapofikiwa hali ya kuaminiana baina ya majirani hao, hii ikiwa ni kulingana na tangazo la ofisi ya Rais Yoon Suk Yeol.
Pendekezo hilo linatarajiwa kupelekwa kwenye baraza la mawaziri kesho Jumanne.
Kusitishwa kwa makubaliano hayo, ambayo tayari yalivunjwa na Korea Kaskazini mwezi Novemba, kunaashiria kuanza tena kwa luteka za kijeshi karibu na mpaka unaozitenganisha Korea hizo mbili, ambazo zilisimama kufuatia makubaliano hayo.