1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin ajadiliana na al-Assad kuhusu mizozo Mashariki ya Kati

25 Julai 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amekutana na Rais Bashar al Assad wa Syria mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4iiki
Syrischer Präsident Baschar al-Assad und Wladimir Putin
Picha: Valeriy Sharifulin/IMAGO/SNA

Putin amesema wamejadiliana juu ya kuongezeka kwa mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mkutano wao wa jana jioni ulifanyika katika wakati ambapo Urusi iliyoisaidia serikali ya Assad wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2015, inaweza kuwa mpatanishi katika mvutano kati ya Syria na Uturuki.

"Tuna fursa ya kuzungumza kwa upana juu ya ugumu wa mahusiano yetu; hatujaonana kwa muda mrefu. Bila shaka, napendelea sana  kusikia maoni yako kuhusu hali inavyoendelea katika kanda nzima. Kwa bahati mbaya hali inaendelea kuzorota na tunaiona ambapo Syria inaguswa moja kwa moja. Kuhusu biashara na uchumi wetu yapo maswali mengi katika seekta hizo. Natumai kwamba hayo pia tunaweza kuyajadili," alisema Putin.

Mkutano huu wa kwanza tangu mwezi Machi mwaka uliopita unafanyika baada ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuondoa uwezekano wa viongozi hao watatu kukutana ili kujaribu kurejesha uhusiano kati ya Ankara na Damascus.