1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Putin aishtumu Ukraine kujaribu kushambulia kinu cha nyuklia

22 Agosti 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameishtumu Ukraine kwa kujaribu kukishambulia kinu cha nyuklia cha Urusi cha Kursk katika mashambulizi yaliofanywa usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4jnY4
Rais wa Urusi Vlamir Putin
Rais wa Urusi Vlamir PutinPicha: Vyacheslav Prokofyev/picture alliance

Urusi imesema kuwa tayari imeliarifu shirika la kimataifa la nishati ya nyuklia IAEA kuhusu hali hiyo na kwamba litatuma wataalamu wake katika kinu hicho kufanya tathmini.

Kaimu gavana wa jimbo la Kursk Alexei Smirnov amemfahamisha Putin kwamba hali iko "imara” katika kinu hicho.

Baadhi ya wakaazi wa Kursk waliohamishwa na mashambulizi ya Ukraine.
Baadhi ya wakaazi wa Kursk waliohamishwa na mashambulizi ya Ukraine.Picha: Nick Connolly/DW

Soma pia: Urusi imesema majeshi yake yameiteka sehemu kubwa ya jimbo la Donetsk.

Putin hata hivyo hakutoa maelezo wala ushahidi kuunga mkono madai yake kwamba Ukraine inalenga kukishambulia kinu hicho cha nyuklia cha Kursk.

Ukraine kwa upande wake haikutoa maoni mara moja kuhusu madai ya Putin wala shirika la habari la Reuters halikuthibitisha kwa njia huru kutokea kwa shambulio hilo.