1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Majeshi ya Urusi yaiteka sehemu muhimu ya Donetsk.

20 Agosti 2024

Majeshi ya Urusi yamesema yameiteka sehemu muhimu ya mashariki mwa Ukraine inayoitwa New York.

https://p.dw.com/p/4jhiX
Kifaru | Ukraine
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye kifaru, katika harakati za kupambana na uvamizi wa Urusi Picha: Jose Colon/Anadolu/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema majeshi yake yameiteka sehemu kubwa muhimu katika jimbo la Donetsk.

Kutekwa kwa mji huo wenye watu 10,000 ni katika jumla ya hatua za Urusi za kusonga mbele mashariki mwa Ukraine.

Urusi imesema majeshi yake pia yameuteka mji wa Zalizne katika jimbo la Donetsk ambalo ni miongoni mwa manne, Urusi ilidai kuyateka mnamo mwaka 2022.

Kwa upande wake majeshi ya Ukraine yalivuka mpaka na kuingia ndani ya jimbo la Urusi la Kursk wiki mbili zilizopita, hatua ambayo Ukraine ilitumai kupunguza shikikizo la majeshi ya Urusi.

Hata hivyo majeshi ya Urusi yamesonga mbele kwenye jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukraine.