1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Polisi wachunguza vito vya thamani vya Bolsonaro Brazil

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Polisi na waendesha mashtaka nchini Brazil wanachunguza ikiwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jair Bolsonaro, alijaribu kuingiza kinyemela vito vya thamani kutoka Saudi Arabia

https://p.dw.com/p/4PEjg
Brasilien Sao Paolo | Zoll beschlagnahmt Diamantschmuck der Regierung von Saudi-Arabien für Michelle Bolsonaro
Picha: Amanda Perobelli/REUTERS

Moja ya seti za vito hivyo vya thamani iliyowasili Brazil Oktoba 2021 inayojumuisha mkufu, hereni na saa, vilipitia uwanja wa ndege wa Sao Paulo vikiwa na aliyekuwa mshauri wake wa migodi na nishati, Bento Albuquerque.

Soma zaidi:Viongozi wa dunia walaani uvamizi wa majengo ya serikali Brazil

Mamlaka za ushuru zilikamata vito hivyo vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3. Kwa mujibu wa Alburqueque, vito hivyo vya thamani vilikuwa kwa ajili ya mke wa Bolsonaro, Michelle.

Aliyewahi kuwa Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro
Aliyewahi kuwa Rais wa Brazil, Jair BolsonaroPicha: Roberto Schmidt/AFP/Getty Images

Gazeti la nchini humo la O Estado de S.Paulo limesema, seti nyingine ya vito vya thamani vya Bolsonaro ni pamoja na saa inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani 150,000.