Polisi wa Kenya wafyatua mabomu ya machozi kwa waandamanaji
25 Juni 2024Tukio hilo linatokea wakati huu ambapo duru zinaeleza kunafanyika maandamano ya taifa zima kupinga mswada wa nyongeza ya kodi.
Kumeripotiwa msururu mkubwa wa polisi katika jiji la kibiashara la Nairobi huku maafisa wa polisi waliovalia mavazi ya kutuliza ghasia wakiwazuia watu kuingia bungeni, ambapo wabunge wanajadili mswada tata wa fedha wenye mapendekezo ya kodi.
Rais wa Kenya asema yuko tayari kuzungumza na Gen-Z
Kwingineko, umati wa watu ulikuwa ukiandamana katika mji wa bandari wa Mombasa, katika ngome ya upinzani ya Kisumu, na ngome ya Ruto huko Eldoret.
Maandamano hayo ambayo hasa yanaongozwa na vijana maarufu kama Gen-Z yalioanza juma lililopia, yameicha bumbuwazi serikali ya Rais William Ruto, huku kiongozi huyo wa Kenya akisema mwishoni mwa juma kwamba yuko tayari kuzungumza na waandamanaji.