1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi UK yakamata zaidi ya watu 1,000 kuhusiana na vurugu

14 Agosti 2024

Maafisa nchini Uingereza wamesema polisi imewakamata watu zaidi ya 1,000 kuhusiana na fujo zilizotokea katika muda wa wiki mbili zilizopita huko England.

https://p.dw.com/p/4jQw9
Uingereza | Maandamano ya wafuati wa itikadi kali za mrengo wa kulia
Baraza la wakuu wa polisi UK limesema watu zaidi ya 1,000 wamekamatwa kuhusiana na vurugu za wafuasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia.Picha: Muhammed Yaylali/Anadolu/picture alliance

Watu wasiopungua 575 wameshatakiwa, huku mahakama zikiendelea kuwashughulikia walioshiriki fujo hizo zilizoikumba miji kadhaa ya England na Ireland Kaskazini, kufuatia vifo vya wasichana watatu waliochomwa kisu Julai 29.

"Vikosi kote nchini hivi sasa vimekamata watu zaidi ya 1,000 kuhusiana na vurugu za hivi karibuni na fujo," Baraza la wakuu wa polisi ya taifa, NPCC, lilisema kupitia mtandao wa X.

UK| Vurugu za wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia
Uingereza pia imewafunga baadhi ya watu wanaoeneza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.Picha: Jordan Pettitt/empics/picture alliance

Fujo hizo za wafuasi wa itikadi kali zilifuatia taarifa za upotoshaji kuhusu utambulisho wa mshukiwa wa shambulio hilo la kisu, ambapo pia watu kadhaa wamefungwa jela kwa kueneza chuki mtandaoni katika siku za karibuni.

Soma pia: Mfalme Charles III azungumzia maandamano ya vurugu Uingereza

Mahakama ya Uingereza inapitia kwa haraka kesi za mahakama na kutoa hukumu za vifuno virefu baada ya machafuko kutulia kabla ya wikendi na serikali imeapa kuwachukulia hatua kali waliohusika.