1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles III azungumzia maandamano ya vurugu Uingereza

10 Agosti 2024

Mfalme Charles III amezungumza kwa mara ya kwanza kufuatia ghasia zilizoitikisa miji ya Uingereza na kusifu kazi ya maafisa wa polisi na huduma za dharura waliodhibiti maandamano ya vurugu na kurejesha hali ya utulivu.

https://p.dw.com/p/4jKAJ
Mfalme Charles III wa Uingereza
Mfalme Charles III wa Uingereza Picha: Ben Stansall/AFP

Mfalme na Malkia Camilla wametoa pia salamu zao za rambirambi kwa familia za wasichana watatu waliouawa katika shambulio la kisu la Julai 29.

Msemaji wa Kasri la Buckingham amesema kuwa Mfalme anatumai kuwa maadili ya pamoja ya kuheshimiana na maelewano yataendelea kuimarisha na kuliunganisha taifa la Uingereza.

Maelfu wajitokeza Uingereza kuonyesha mshikamano dhidi ya ubaguzi wa rangi

Mamia ya watu walikamatwa kufuatia maandamano hayo yaliyogeuka kuwa ya kupinga wahamiaji na waislamu.