MigogoroHaiti
Haiti: Polisi waendelea kukabiliana na magenge ya wahalifu
17 Machi 2024Matangazo
Polisi wamesema wamefanikiwa kuondoa vizuizi na kuwaua majambazi kadhaa wakati wa operesheni yao katika mtaa wa Delmas.
Hata hivyo vurugu zinaendelea katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince ambako magenge yanadhibiti asilimia 80 ya mji huo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF limesema moja ya kontena lake lililokuwa limebeba vifaa muhimu liliporwa na magenge katika bandari kuu ya Haiti.
Soma pia: Hofu yatanda Haiti katikati ya mkwamo wa kisiasa
Shirika la kikanda CARICOM, Umoja wa Mataifa na Marekani wanaunga mkono kuanzishwa kwa baraza la mpito ili kuchukua nafasi itakayoachwa na Waziri Mkuu Ariel Henry, ambaye alitangaza Jumatatu kuwa angejiuzulu mara baada ya kuundwa kwa baraza hilo la kisiasa.