1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Hofu yatanda Haiti katikati ya mkwamo wa kisiasa

16 Machi 2024

Hali ya wasiwasi imetanda katika mji mkuu wa Haiti huku vurugu zikienea katika sehemu mbalimbali za mji huo baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Ariel Henry na kutokuwepo kwa mpango madhubuti wa kisiasa kujaza nafasi yake.

https://p.dw.com/p/4dnfk
Polisi ya Haiti ikishika doria
Polisi ya Haiti ikishika doriaPicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Mwandishi wa habari la shirika la AFP amesema kuwa vurugu zimeshuhudiwa usiku kucha huku magenge yakilenga uwanja wa ndege na nyumba ya afisa mwandamizi wa polisi.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa, polisi walikabiliana na magenge ya wahalifu katika eneo la Delmas, ambalo linachukuliwa kuwa ngome ya kundi la wahalifu la G9 linaloongozwa na Jimmy Cherizier almaarufu kama "Barbeque."

Soma pia: Majina mengi ya Baraza la mpito nchini Haiti yawasilishwa 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken jana alisema kuwa, wengi wa wajumbe ambao watakaa kwenye baraza la mpito la kisiasa tayari wametajwa na makundi watakayoyawakilisha.

Wizara hiyo ya mambo ya nje ilieleza matarajio yake kwamba wajumbe wa baraza hilo la mpito watateuliwa katika muda wa saa 24 hadi 48 zijazo, japo mchakato huo umechelewa. Baraza hilo limetwika jukumu la kumchagua waziri mkuu wa muda ambaye atateua serikali ijayo jumuishi.