Poland kuimarisha ukaguzi wa wahamiaji mpakani na Slovakia
26 Septemba 2023Serikali ya Poland imeagiza imeagiza kuimarishwa kwa ukaguzi katika mpaka wa nchi hiyo na jirani yake Slovakia katikati ya ongezeko wahamiaji wanaoingia Ulaya na nchini humo.
Waziri mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki amesema jana kwamba hatua hiyo inayalenga zaidi mabasi na magari yanayodhaniwa kusafirisha wahamiaji haramu. Amesema hayo katika mkutano wa kampeni mjini Krasnik.
Amesema hatua hizo pia zinanuia kuwaonyesha wale wanaodai kwamba mipaka ya Poland ina mianya inayoruhusu wahamiaji kuingia na kuongeza kuwa huko nyuma wahamiaji waliingia Poland kupitia Hungary na Slovakia inayopakana nayo upande wa kusini.
Eneo la mpaka wa Poland na Slovakia lina urefu wa kilomita 540 na wanachama hao wa Umoja wa Ulaya ni sehemu ya eneo la visa ya Ulaya, maarufu Schengen.