1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Pistorius asifu mafunzo ya vikosi vya Ukraine, Ujerumani

30 Mei 2024

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema mafunzo yanayotolewa kwa vikosi vya Ukraine juu ya mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot nchini Ujerumani ni mchango muhimu katika kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi

https://p.dw.com/p/4gR51
Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ujerumani aina ya Patriot katika uwanja wa ndege wa Vilnius kabla ya mkutano wa kilele wa NATO huko Vilnius, Lithuania mnamo Julai 10,2023
Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ujerumani aina ya PatriotPicha: Ints Kalnins/REUTERS

Wakati wa ziara yake jana kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi kaskazini mwa Ujerumani, Pistorius alisema mifumo ya ulinzi wa anga ndio inayotegemewa zaidi na Ukrainekwa sasa, na kuongeza kuwa ni ishara muhimu kwa nchi hiyo kwamba Ujerumani iko upande wake.

Soma pia;Ujerumani kuipatia Ukraine mfumo wa ziada wa ulinzi wa anga

Mkuu wa kikosi hicho cha Ukraine kinachopokea mafunzo aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, amesema mafunzo hayo yangeweza tu kufanywa kwa ufanisi nje ya Ukraine na hafikirii ni jambo la busara kuhamisha mafunzo hayo kutoka Ujerumanihadi Ukraine.