1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO:Ujerumani yakubali kutuma mifuno ya ulinzi anga Ukraine

Hawa Bihoga
7 Oktoba 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg ameupongeza uamuzi wa Ujerumani wa kupeleka mfumo mwingine wa ulinzi wa anga aina ya Patriot nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4XEwB
Rais wa Ukraine Volodymiyr Zelensky akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Rais wa Ukraine Volodymiyr Zelensky akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Stoltenberg ameyasema hayo na kuongeza kuwa anaelewa wasiwasi wa Berlin juu ya kutotaka kuwa sehemu ya mzozo huo.

Katibu Mkuu huyo waNATOameliambia gazeti la Welt am Sonntag kwamba anaelewa msaada wa NATO kwa Ukraine una hatari ya kuongeza mvutano, lakini ameitaja hatari hiyo kuwa ni ndogo kuliko kuruhusu rais wa Urusi Vladmiry Putin kushinda vita hivyo vilivyodumu kwa takriban miezi 20 sasa.

Soma pia:Ujerumani: NATO yapaswa kujiimarisha kufuatia vita Ukraine

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alitumia suala la hatari ya kuongezeka kwa mvutano kuuhalalisha uamuzi wake wa kutokupeleka makombora aina ya Taurus yanayoweza kusafiri hadi umbali wa kilomita 500 kwenye uwanja wa vita, licha ya maombi ya dharura ya Ukraine.