1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis atoa mwito wa msaada zaidi kwa wagonjwa wa mpox

26 Agosti 2024

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani ametoa mwito kwa serikali na kampuni za kutengeneza dawa duniani kufanya kazi ya ziada ili kupeleka chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya nyani kwa mataifa yaliyoathirika na ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/4ju0C
Reisende Päpste | Bangui (2015)
Papa Francis akiwaombea watoto alipofanya ziara katika kambi ya wakimbizi mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati.Picha: L'Osservatore Romano/AP Photo/picture alliance

Papa Francis amesema anawaombea watu wote walioambukizwa wapate afueni ya haraka, hasa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliokutwa na ugonjwa wa homa ya nyani.

Shirika la afya duniani WHO mwezi huu lilitangaza ugonjwa wa homa ya nyani uliosambaa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na baadhi ya mataifa ya Afrika kuwa dharura ya afya ya umma kimataifa.

Soma pia: Uganda yaripoti visa vingine viwili vya Mpox

WHO imehimiza kutengenezwa na kusambazwa kwa chanjo zaidi dhidi ya ugonjwa huo.

Mpox imeenea zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imesababisha vifo vya zaidi ya watu 570 mwaka huu. Mlipuko wa ugonjwa huo pia umeripotiwa nchini Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na mgonjwa wa kwanza wa mpox aliripotiwa nchini Sweden wiki iliyopita.