1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa atoa wito wa kusitishwa kwa safari za vifo

5 Machi 2023

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, ametoa wito wa kusitishwa usafirishaji haramu wa watu, wiki moja baada ya boti moja kuzama Kusini mwa Italia na kusababisha vifo vya watu 70.

https://p.dw.com/p/4OHAT
Papst Franziskus I Weihnachtsbotschaft „Urbi et Orbi"
Picha: Yara Nardi/REUTERS

Katika maombi yake kwenye uwanja wa St Peters, Papa aliye na miaka 86, amesema anaomba safari hizo za matumaini zisigeuke tena na kuwa safari za vifo na maji katika bahari ya maditerenia yasijae damu kufuata matukio yanayoshuhuiwa hivi karibuni. 

Shughuli za uokozi zinaendelea baada ya mkasa wa boti ya wahamiaji kuzama

Vijana 15 waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 walipoteza maisha katika ajali iliyotokea wiki iliyopita katika mkoa wa Croton katika pwani ya Italia. Kundi la uokozi bado linaedelea kutafuta miili na manusura wa ajali hiyo. 

Vyombo vya hbaari vya Italia vimeripoti kwamba washukiwa watatu wanaofanya kazi hiyo ya kuwasafirisha watu kwa njia haramu.