SiasaAsia
Pakistan yaanza kuwazika wahanga zaidi ya 50 wa ugaidi
31 Julai 2023Matangazo
Mashambulizi hayo ya siku ya Jumapili (Julai 30) yaliwajeruhi watu wengine zaidi ya 200.
Hakukuwa na kundi lililodai kuhusika lakini mamlaka za Pakistan ziliapa kuwasaka wote waliopanga hujuma hiyo.
Kwenye mashambulizi hayo, mtu mwenye mabomu alijiripua katikati ya mkutano wa wafuasi wa chama cha Jamiat Ulema-e-Islam kinachoongozwa na mwanasiasa na kiongozi wa dini mwenye misimamo mikali, Fazlur Rehman.
Soma zaidi: Watu 44 wauawa, 200 wajeruhiwa Pakistan
Hata hivyo, mwazuoni huyo hakuhudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye soko moja katika wilaya ya Bajur karibu na mpaka wa Afghanistan.
Polisi ilisema uchunguzi wao wa awali unaashiria genge lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu ndiyo limehusika.