1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Watu 44 wauawa, 200 wajeruhiwa Pakistan

31 Julai 2023

Watu 44 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitowa muhanga kujiripuwa katika eneo lililo kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan na lililokuwa ngome ya kundi la Taliban.

https://p.dw.com/p/4UaKF
Maulana Fazlur Rehman | Mitglied der pakistanischen Nationalversammlung
Picha: Rizwan Tabassum/AFP/Getty Images

Wilaya ya Bajur iliyo karibu na mpaka wa Afghanistan ilikuwa ngome ya Wataliban wa Pakistan, washirika wa karibu wa serikali ya Taliban nchini Afghanistan, kabla ya jeshi la Pakistan kuwafurusha wanamgambo hao katika eneo hilo.

Wafuasi wa muhubiri wa Kipakistan mwenye msimamo mkali na kiongozi wa chama cha kisiasa, Maulana Fazlur Rehman, ambaye chama chake cha Jamiat Ulema-e-Islam kinawaunga mkono wanamgambo wa itikadi kali wa eneo hilo, walikuwa mkutanoni kwenye ukumbi uliokuwa karibu na soko nje ya mji mkuu wa wilaya hiyo.

Hata hivyo, maafisa wa chama walisema Rehman hakuwapo katika mkutano huo.