1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Orbán atangaza muungano mpya wa mrengo wa kulia

30 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán ametangaza kuunda muungano na vyama vyenye umaarufu mkubwa kutoka Austria na Jamhuri ya Czech katika ngazi ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4hh3o
Neues rechtspopilstisches Bündnis in EU-Parlament
Mwenyekiti wa ANO Andrej Babis, mwenyekiti wa chama cha shirikisho Herbert Kickl (FPÖ) na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban.Picha: TOBIAS STEINMAURER/APA/picturedesk.com/picture alliance

Muungano huo uliopewa jina la Patriots for Europe, unaunda kikundi kipya cha mrengo wa kulia katika Bunge la Ulaya.

Soma pia: Orbán kufanya uhamiaji kuwa lengo la urais wa Hungary kwa Umoja wa Ulaya

Patriots for Europe imeundwa na chama cha Orbán cha Fidesz, Freedom Party of Austria (FPÖ) na chama cha Jamuhuri ya Czech cha Republic's Action of Dissatisfied Citizens.

Orbán amesema muungano huo unatarajia kupata wafuasi zaidi hivi karibuni ili kuwa kile alichokiita "kundi kubwa zaidi la vyama vya mrengo wa kulia baraniUlaya."

Hungary itachukua nafasi ya kupokezana ya urais wa Baraza la Umoja Ulaya siku ya Jumatatu hadi mwisho wa mwaka.