1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Xi kufanya mazungumzo na Orbán nchini Hungary

9 Mei 2024

Rais wa China Xi Jinping anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán mjini Budapest leo. Hungary ndio kituo cha mwisho katika safari yake Ulaya, ambayo awali ilimfikisha Ufaransa na Serbia.

https://p.dw.com/p/4ffR4
Rais wa China  Xi Jinping akilakiwa na mwenzake wa Serbia Aleksandar Vucic
Rais wa China Xi Jinping akilakiwa na mwenzake wa Serbia Aleksandar VucicPicha: Serbian Presidential Press Service/AP/picture alliance

Hungary ni nchi pekee ya Umoja wa Ulaya ambayo imehusishwa katika mradi mkubwa wa miundombinu na uwekezaji wa China. Kutokana na urafiki na serikali ya Beijing, Orbán anataka kuweka hali ya uzanikatika mataifa ya Umoja wa Ulaya, eneo ambaro mara nyingi anaonekana kutengwa.

Soma pia:China na Serbia zatia saini makubaliano ya pamoja

China inajenga  reli yenye urefu wa kilomita 350 kati ya mji mkuu wa Hungary Budapest na mji mkuu wa Serbia Belgrade. Katika taifa hilo kadhalika China inajenga kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa magari ya umeme na betri zake.