1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Nigeria yapitisha bajeti ya magari ya kifahari kwa wabunge

3 Novemba 2023

Wabunge wa Nigeria wameidhinisha bajeti ya kwanza ya ziada ya serikali mpya, ambayo inajumuisha marupurupu makubwa ya magari ya kifahari na nyumba kwa ajili ya rais, mke wake na maafisa wengine wa umma

https://p.dw.com/p/4YNt3
Rais wa Nigeria  Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Temilade Adelaja/REUTERS

Uamuzi huo umezusha hasira na ukosoaji mkubwa kutoka kwa raia.

Katika bajeti hiyo, serikali ilikuwa imetenga takriban dola milioni 38 kwa ajili ya ndege za rais, magari na ukarabati wa nyumba za makazi za ofisi ya rais, makamu wa rais na mke wa rais, ingawa ofisi yake haitambuliwi kikatiba.

Rais wa Nigeria atangaza nyongeza ya muda ya mishahara

Kabla ya bajeti hiyo kuidhinishwa, wabunge waliondoa dola milioni 6.1 zilizokuwa zimepangwa awali kwa ajili ya boti la kifahari la rais na kuihamishia pesa hiyo kwenye mikopo ya wanafunzi.

Zaidi ya wabunge 460 wa shirikisho, kila mmoja atapata gari linalokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola laki moja na nusu 150,000 kwa gari moja.