1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaingia makubaliano ya kusambaza gesi Ujerumani

22 Novemba 2023

Nigeria imesema imeingia makubaliano na Ujerumani ya ugavi wa nishati ya gesi na Ujerumani kuwekeza dola milioni 500 katika nishati endelevu, katika taifa hilo ambalo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4ZItZ
Berlin, Ujerumani | Kansela Olaf Scholz na Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria
Berlin, Ujerumani | Kansela Olaf Scholz na Rais Bola Ahmed Tinubu wa NigeriaPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Mkataba huo umetiwa saini na kampuni ya gesi ya Nigeria Riverside LNG  na kampuni ya nishati ya Ujerumani ya Johannes Schuetze.

Soma pia:Ziara ya Scholz Afrika na shauku ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi

Nigeria inatarajiwa kufanya usambazaji wake wa kwanza wa gesi kwa Ujerumani mwaka 2026. Ujerumani pia iko katika majadiliano na kampuni ya Siemens ili kuisaidia Nigeria katikausambazaji wa nguvu za umeme ambao unasuasua na umekuwa mzigo mkubwa kwa Wanigeria na wafanyabiashara nchini humo.