1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yaziidhinisha Mali, Burkina Faso kuisaidia kijeshi

25 Agosti 2023

Niger imeidhinisha kuingilia kati kwa majeshi ya Mali na Burkina Faso iwapo itavamiwa, ishara kwamba utawala wa kijeshi ya Niamey hauko tayari kukubaliana na matakwa ya kuondoka madarakani yanayotolewa na ECOWAS.

https://p.dw.com/p/4VZQ9
Niger | General Abdourahmane Tiani
Picha: Balima Boureima/Reuters

Haya yamesemwa katika taarifa ya pamoja  baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu katika mji mkuu wa Niger, Niamey, kujadili kuongeza ushirikiano katika masuala ya usalama na mambo mengine ya pamoja.

Soma zaidi: Niger yaidhinisha wanajeshi wa Mali na Burkina Faso

Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imekuwa ikijaribu kujadiliana na viongozi wa kijeshi walioongoza mapinduzi ila ilionya kwamba iko tayari kutuma vikosi nchini Niger kurudisha demokrasia iwapo diplomasia haitofanikiwa.