1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu amfuta kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant

6 Novemba 2024

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amemfuta kazi waziri wake wa ulinzi, Yoav Gallant, na kusema amekosa imani naye. Haya ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya waziri huyo mkuu.

https://p.dw.com/p/4mfnn
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kushoto) na waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant  (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari katika kambi ya kijeshi ya Kirya mjini Tel Aviv mnamo Oktoba 28, 2023
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kushoto) na waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant (kulia)Picha: ABIR SULTAN/AFP

Netanyahu amesema ingawa kulikuwa na uaminifu kati yao katika miezi ya kwanza ya vita na ushirikiano wao ukapata ufanisi, uaminifu huo kwa bahati mbaya umevunjika katika miezi ya hivi karibuni.

Waziri huyo mkuu pia ameongeza kuwa Gallant alifanya maamuzi na kutoa taarifa zilizoenda kinyume cha maamuzi ya baraza la mawaziri.

Gallant aonya kuhusu ukosefu wa maadili nchini Israel

Gallant ametoa taarifa yake na kusema usalama wa taifa la Israel siku zote umekuwa na daima utabaki kuwa jukumu la maisha yake.

Gallant pia ameonya kuhusu ukosefu wa maadili nchini humo.

Nafasi ya Gallant inatarajiwa kuchukuliwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Israel Katzis.

Upinzani nchini humo umeikosoa hatua ya Netanyahu huku kiongozi wake Yair Lapid akisema kumfuta kazi Gallant katikati ya vita ni kitendo alichokiita cha wazimu na kutoa wito kwa Waisraeli kuandamana.