1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Yoav Gallant aunga mkono kuachiliwa mateka

10 Septemba 2024

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema kuwa anaunga mkono kuachiliwa kwa mateka katika awamu ya kwanza ya makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4kTWk
Israel Jerusalem | Yoav Gallant na Armee Herzi Halevi
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant (kushoto) alipohudhuria sherehe za ukumbusho wa wanajeshi waliouawa wakati wa vita vya Gaza 2014Picha: Abir Sultan/AFP/Getty Images

Gallant ameongeza kuwa makubaliano hayo yataipatia Israel, fursa ya kimkakati ya kushughulkia masuala mengine ya kiusalama.

Akizungumza na waandishi wa habari wa kigeni, waziri huyo wa ulinzi amesema suala la kuwarejesha nyumbani mateka ndio jambo sahihi la kufanya.

Ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuendelea kuishinikiza Hamas kufikia makubaliano, na kuunga mkono kwa dhati hatua ya kwanza ya makubaliano ya awamu tatu ya kusitisha mapigano yaliyotangazwa na Rais wa Marekani Joe Biden mnamo Mei 31.

Wakati huohuo wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas, imesema hadi kufikia sasa watu waliouawa katika mapigano imefikia watu 41,020.