1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSyria

Ndege za msaada Syria zabadilishwa njia baada ya shambulizi

Daniel Gakuba
7 Machi 2023

Wizara ya usafirishaji ya Syria imesema inazibadilishia njia ndege zinazobeba msaada wa wahanga wa tetemeko la ardhi, baada ya shambulio la anga la Israel lililouharibu uwanja wa ndege wa Aleppo jana usiku.

https://p.dw.com/p/4OKqW
Syrien | Erdbeben-Hilfslieferung der EU in Damaskus angekommen
Picha: Syrian Arab Red Crescent/Handout/REUTERS

Tangazo la wizara hiyo limesema ndege hizo sasa zitaelekezwa katika mji mkuu, Damascus na Latakia kaskazini magharibi mwa Syria.

Tangu kutokea tetemeko kubwa la Februari 6, dazeni kadhaa za ndege kutoka Mashariki ya Kati na Ulaya na kwingineko zimekuwa zikiwasili Syria zikiwa na msaada kwa wahanga.

Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulizi hilo kwenye uwanja wa Aleppo.