1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Anayeshukiwa kuripua bomu Istanbul, Uturuki auwawa

24 Februari 2023

Vikosi vya Uturuki vimemuua mtu anayedaiwa kuwa ndie mpangaji mkuu wa shambulizi la bomu huko mjini Istanbul katika oparesheni kaskazini mwa Syria.

https://p.dw.com/p/4Nwvj
Türkei Explosion in Istanbul
Picha: YASIN AKGUL/AFP/Getty Images

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba, katika oparesheni ya maafisa wa kijasusi iliofanyika Februari 22 kwenye mji wa Qamishli mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Halil Menci hakuwa na mafungamano na upande wowote.

Katika shambulio la bomu la Novemba 13 mwaka uliopita kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi mjini Istanbul watu sita waliuwawa wakiwemo watoto wawili, na wengine zaidi ya 80 walijeruhiwa.

Takriban watu 17 wapo kizuizini kufuatia mkasa huo wakisubiri kusomewa mashatka akiwemo mwanmke mmoja wa Syria aliyeshutumiwa kubeba bomu.

Mamlaka za Uturuki zimekuwa zikikishutumu chama cha wafanyakazi cha Wakurdi PKK, pamoja na makundi ya Wakurdi wa Syria yenye mafungamano nayo. Wanamgambo wa Kikurdi wamekuwa wakikanusha kuhusika na tukio hilo.