Nchi za Magharibi zahimiza utulivu baada ya uchaguzi Kongo
24 Desemba 2023Matangazo
Hatua hiyo inatokea baada ya viongozi watano kutoka vyama vya upinzani nchini humo katika taarifa yao ya pamoja kuitisha maandamano siku ya Jumatano.
Balozi 12 ya mataifa ya Ulaya na Ubalozi wa Kanada katika taarifa ya pamoja wametoa wito kwa Wakongomani kuwa watulivu wakati huu ambapo zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea.
Soma pia:Wagombea wa upinzani Kongo wanapanga maandamano ya kupinga uchaguzi wa rais
Takriban watu milioni 44 katika taifa hilo lenye watu milioni 100 walijiandikisha kupiga kura, huku zaidi ya wagombea 100,000 wakiwania nyadhifa mbalimbali. Rais Felix Tshisekedi anagombea muhula wake wa pili dhidi ya wagombea wengine 18 wa upinzani.